ZOEZI LA MAOMBI YA PASIPOTI LINAENDELEA

Maofisa wa Uhamiaji ambao wako rasmi kutatua matatizo ya pasipoti kwa watanzania , wakiwa  katika siku ya pili ya zoezi hilo,ambalo linaanzia asubuhi mapema saa 3 hadi saa kumi na mbili jioni.










Ofisa wa uhamiaji akisaini kitabu cha wageni wa Jumuiya ya Watanzania Italia.

Ofisa wa uhamiaji akisaini kitabu cha wageni wa Jumuiya ya Watanzania Italia.



Maofisa wa Uhamiaji kutoka Dar Es Salaam na Zanzibar wameanza zoezi la kupokea maombi ya pasipoti kutoka kwa Watanzania waliopo Italy. Maofisa hao wanategemewa kuelekea Turkey na Greece,kwa ajili hiyo hiyo. Haya ni matunda ya Kamati ya Diaspora iliyokutana na Mh Balozi James Alex Msekela, mwezi juni mwaka huu. Kamati ilikutana na balozi na maofisa wa juu wa kibalozi kwa ajili ya kutambulisha kamati na uongozi wake,na pia kuwakilisha kero na matatizo ya watanzania wanaoishi Italy . Mkutano huo uliisha kwa mafanikio makubwa. Kwa hiyo haya ni matokeo ya uchapa kazi wa kweli wa mh Balozi Dkt James Alex Msekela, kwani katika mapumziko yake nchini Tanzania mwezi August mwaka huu alitumia muda wake kukutana na Kamishna wa Uhamiaji Tanzania kujadili suala la matatizo ya Pasipoti kwa watanzania wa Maeneo ya uwakilishi wake.

Post a Comment

0 Comments